Benard Membe afariki dunia, aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.

Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.

Screenshot_2023-05-12-11-23-16-709_com.instagram.android.jpg

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *