download - 2022-04-10T134807

Ukraine - NATO: Jens Stoltenberg amesema kuwa jumuiya hii itapeleka kikosi kamili cha kijeshi katika upande wa mashariki ili kujihami dhidi ya Urusi

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema kuwa jumuiya hiyo itapeleka kikosi kamili cha kijeshi katika upande wa mashariki ili kujihami dhidi ya Urusi. 

Hatua hiyo inakuja kufuatia kampeni ya kijeshi ya Moscow nchini Ukraine.

Katika mahojiano yaliyochapishwa na gazeti la The Telegraph siku ya Jumamosi, Stoltenberg alieleza kuwa kambi ya kijeshi inayoongozwa na Marekani imezingatia "mabadiliko ya kimsingi" ili kuakisi vyema "ukweli mpya" huko Ulaya.

"Sasa tumewauliza makamanda wetu wa kijeshi kutoa chaguzi kwa kile tunachoita kuweka upya, marekebisho ya muda mrefu zaidi ya NATO," alisema, akiongeza kuwa maamuzi juu ya suala hilo yanatarajiwa katika mkutano wa kilele wa umoja huo utakaofanyika mwezi Juni huko Madrid, Uhispania.

Picha ya AFP rejeo letu ikionesha Wanajeshi wa Marekani wakiwa Arlamow, Poland, Machi 3, 2022.

 


Comment As:

Comment (0)